Maandalizi ya kupokea Ugeni mkubwa wa Marais wawili John Pombe Magufuli wa Tanzania na Museveni wa Uganda yanaendelea vizuri jijini Tanga. Na hii ni katika uwekaji jiwe la msingi la mradi huo mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka CHONGOLEANI TANGA hadi nchini Uganda katika eneo la HOIMA.
Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa maeneo yote ambayo bomba hili litapita, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na:-
1.Kupata ajira wakati wa ujenzi wa bomba hilo.
2.Kufanya biashara wakati wa ujenzi wa bomba hilo.
3.Wataalamu wenye fani ya mafuta kupata ajira katika mradi huo.
4.Watanzania kufaidika na mradi huu kwa kupata nishati hii kwa bei nafuu.
Marais wetu hawa JPM na MUSEVENI watazindua mradi huu siku ya jumamosi kwa kuweka jiwe la msingi ikiwa ni kiashiria cha kuanza ujenzi huu wa bomba la mafuta. Zoezi hili litafanyika huku likihudhuriwa na mamia ya watanzania na waganda huku mamilioni ya watazamaji kutoka Uganda na Tanzania wakifuatilia tukio hili kupitia vituo mbalimbali vya Televisheni zao na wengine wakisikiliza kupitia vituo vya redio. Hakika tukio hili litakuwa la kihistoria kwa nchi zote mbili.
MUNGU IBARIKI AFRIKA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU WABARIKI VIONGOZI WETU WAKAFANIKISHE TUKIO HILI LA KIHISTORIA.
EmoticonEmoticon