Tuesday, August 15, 2017

MASHABIKI WA DIAMOND PLATINUM WAZIDI KUHOJI JUU YA BABA HALALI WA MTOTO WAKE WA KIUME

Mashabiki wa Msanii wa Bongo fleva nchini Diamond Platinum 'Simba' waendeleza mjadala mtaani, wakitaka wawekwe wazi ni kweli huyu mtoto wake wa pili wa kiume aliyezaa na staa wa Uganda "Zari". Hili linaendekea kuwatesa kwani mtoto huyo Inaonekana anafanana zaidi na Mganda ambaye katangulia mbele za haki IVAN na ambaye ni baba wa watoto wawili aliozaa na shemeji yetu Zari. Mtoto huyo ambaye kabebwa na Diamond ukimcheki vizuri utagundua kuwa kafanana na mmoja wa watoto wa Ivan ambaye kafanana zaidi na baba yake Marehemu. Hapa ndipo wanajiuliza inawezekana kijana wao Simba pale kwa Zari kuna kitu kafuata ambacho ni siri yake na hataki amvuruge Zari kabla ya kukipata? Au hawa jamaa ni ndugu wamezaa na Mke mmoja? Mmoja wa mashabiki wa Diamond ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema "Hata wafiche vipi ipo siku ukweli utajulikana tu". Kazi kwako mpenzi msomaji wetu na tunaamini utatupa majibu yako


EmoticonEmoticon