Sunday, August 6, 2017

HATIMAYE PETER MANYIKA ATUA SINGIDA UNITED

Tags


AMEAMUA KUTUA SINGIDA UNITED

Aliyekuwa kipa wa timu ya Simba Sports Club Peter Manyika 'Manyika Jr' ameachana na timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi aliyoitumikia kwa kipindi kirefu na kutua Singida United iliyopanda daraja msimu huu sambamba na Lipuli FC ya Iringa na Mji Njombe ya Njombe ikiwa ni hatua yake ya kutafuta namba kikosi cha kwanza baada ya kukosa ndani ya timu ya Simba ambayo kwa sasa ina makipa Aishi Manula kutoka Azam na Nduda kutoka Mtibwa. Hii inakuja baada ya timu ya Simba kumshauri atafute timu ambayo atapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Mkataba huo ni wa miaka miwili.


EmoticonEmoticon