Friday, August 11, 2017

AZAM FC YAICHAKAZA URA YA UGANDA KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI

Tags

Timu ya soka ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam ambayo iko ziarani Uganda kucheza michezo kadhaa ya kirafiki kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania bara. Leo ilikuwa ni mechi nyingine ya kirafiki kati ya Azam FC na URA ya Uganda, katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Philipo Omondi timu ya Azam imeizamisha URA mabao mawili kwa bila 2-0, na mabao hayo yakifungwa ndani ya kipindi cha kwanza na kipindi cha pili, na kwa matokeo haya Azam inaleta matumaini ya kufanya vizuri katika Ligi kuu msimu huu baada ya kufanya vibaya msimu uliopita. Timu ya Azam FC itakuwa huko Uganda kwa siku kadhaa ikiendelea na Michezo ya kirafiki na timu za nchini humo zinazoshiriki ligi kuu ya Uganda


EmoticonEmoticon