Thursday, August 10, 2017

KUTANA NA KIJANA MCHEKESHAJI KUTOKA JIJINI MBEYA

Tags

Unapozungumzia sanaa ya Vichekesho kwa hapa kwetu Tanzania wengi watawafikiria magwiji kama Kingwendu, Mpoki, Joti, MC Pilipili, Masanja Mkandamizaji, na wengine wengi kama King Majuto. Na hawa wote wamekuwa ni kutoka jijini Dar es Salaam. Kumbe si Dar tu hata mikoani pia kuna vipaji ambavyo havijapewa Sapoti na kuonekana. Hapa namzungumzia kijana kutoka wilayani Chunya katika mkoa wa Mbeya. Kijana huyu si mwingine bali ni Peter Mwakitwange ndo jina alilopewa na wazazi wake na katika sanaa za Vichekesho anajulikana zaidi kwa jina la Mbwene Mzalendo. Kijana huyu anakipaji kikubwa sana ndani yake, anaweza kuiga sauti za watu mbalimbali maarufu nchini wakiwemo viongozi wa kidini, kisiasa, na hata wasanii mbalimbali. Na sauti iliyompa jina jijini Mbeya ni ile ya gwiji la Vichekesho aliyekuwa gumzo kila Kona kwa staili yake ya kuongea, kutembea na kugeuza macho Marehemu Kinyambe mpaka kufikia hatua ya kuitwa Kinyambe Junior na wanaMbeya. Nyota yake ilikuja kung'aa zaidi mwaka juzi 2015 alipokuwa akishiriki kwenye matamasha ya Uzinduzi wilayani Chunya. Na hapa ndipo aliposhauriwa na wadau wa burudani kuwa Chunya si level zake hivyo asogee mbele na ndipo alipoamua kuingia jijini Mbeya mwaka huo huo. Anasema "haikuwa kazi rahisi kuwashawishi wapenda burudani lakini kwa msaada wa rafiki yake kutoka Mzalendo Entertainment ndugu Kibwagizo aliweza kusimama na kupeperusha bendera vilivyo ya mkoa wa Mbeya" .Kupitia sanaa ya Vichekesho ameweza kutoa burudani maeneo yafuatayo;-Arusha, Mbeya, Songwe, Iringa, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Tabora, Njombe nk. Na pia ameweza kufanya kazi na makampuni mbalimbali yakiwamo ya Coca-Cola na Safari lager kwa nyakati tofauti. Anaendelea kusema lengo lake ni kufika mbali zaidi iwapo wadau watajitokeza kumsapoti kama anavyopata Sapoti kutoka kwa wanaMbeya wote na zaidi ni kutoka kwa mfanyabiashara maarufu wa viatu jijini Mbeya ajulikanaye kwa Jina la Thomas Wadox. Hizi ni baadhi ya picha ambazo zinamuonesha akitokea burudani ndani ya viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya maarufu kama NANE NANE siku ya sikukuu ya nane nane.

HAPA NI CHINI YA VODACOM Zifuatazo ni chini ya kampuni ya bia ya SAFARI
Huyo ndiyo Mbwene Mzalendo kutoka jijini Mbeya na sasa amesema anaelekeza nguvu zake jijini Dar es Salaam ambako anaamini ndiyo kuna mafanikio yake zaidi katika sanaa. Taarifa hii na mwandishi wetu


EmoticonEmoticon