Hapa duniani kila mmoja ana ndoto yake, lakini waliowengi huzipuuzia ndoto zao wakiamini kuwa hawawezi kufikia kwa kuwa yeye si wa malengo hayo na hapo huamua kukimbilia ndoto za wengine ambao wanazifanyia kazi. Ndiyo hapa utakuta biashara imeanzishwa leo kesho imekufa ni kwa sababu ulikurupuka pasipo kujua inaendeshwa vipi inahitaji Uvumilivu kiasi gani. Kila mmoja anapaswa kusimamia kwenye ndoto yake hata kama atakutana na vipingamizi namna hautakiwi kukata tamaa. Mfano mzuri ni 'producer' maarufu nchini Tanzania mwenye asili ya nje MIKA MWAMBA, ndoto ilikuwa ni kuwa mzalisha muziki maarufu Tanzania na duniani kote na aliamini katika hilo.
Alianza kutafuta sehemu ambayo itamfikisha kwa kutafuta ajira katika Studio mbalimbali za muziki Tanzania lakini wengi walimdhihaki na kumfukuza kwa kuwa ilikuwa ndoto yake haikumkatisha tamaa aliendelea kupigania ndoto yake. Na mwisho wa siku ndoto yake ilitimia na leo tunamzungumzia.
Hivyo amini katika kile unachokifanya na kukifurahia maishani.
EmoticonEmoticon