Thursday, August 10, 2017

JIFUNZE BIASHARA YA MAYAI YA KUKU WA KIENYEJI

Biashara imekuwa changamoto kubwa nchini kwetu Tanzania.Hii ni kutokana na tatizo la ubunifu wa biashara mpya,kila mtu akitaka kuanzisha biashara hawezi kuanzisha biashara ya kitofauti na nyingine zinazofanyika katika eneo Lake .Kila mmoja anataka kufanya biashara inayofanywa na mwenzake kwa ina watu au wateja wengi. Leo nakuletea biashara isiyohitaji mtaji mkubwa sana ni biashara unayofanya kulingana na Mahitaji ya wateja wako,si biashara nyingine bali ni biashara ya mayai ya kuku wa kienyeji. Kwanza kabisa anza kwa kuangalia ni sehemu gani ya nje ya mji hasa kijijini kuna upatikanaji mkubwa wa mayai haya. Maeneo ya vijijini asilimia kubwa yai moja linauzwa kwa shilingi 300 hadi mawili kwa shilingi 500.Ukipeleka mjini au hata vijijini huko huko kwenye vibanda vya chips utauza yai moja shilingi 500 ambayo ni faida ya shilingi 200 kwa kila yai. Ukinunua mayai elfu moja (1000) ambayo ni sawa na shilingi 300,000/= Mayai 1000@shilingi 300 = shilingi 300,000/=.Hivyo ukiuza yai moja kwa shilingi 500 kwa mayai 1000 itakuwa sawa na shilingi 500,000/=.Shilingi laki tano "500,000" ukitoa laki tatu "300,000" utapata shilingi laki mbili "200,000". Kumbuka hii ni faida kubwa sana. Mayai 1000 ni sawa na trei 33 ambazo utakusanya na kuuza ndani ya siku 14. Katika mwezi kuna siku 30 sawa na wiki 4. Faida hii ya 200,000/=kwa wiki mbili mara ni sawa na shilingi 400,000/=hii ni kwa mwezi mmoja. Inakuwaje, chukulia kwa siku unakusanya mayai 80 kwa siku x siku 14 sawa na Mayai 1120, hivyo kwa wastani tufanye mayai 1000. Hivyo kiasi hiki cha 400,000 /= ni mwezi mmoja, je kwa miezi kumi na mbili sawa na shilingi ngapi? Itakuwa ni 400,000 x 12 = 4,800,000/= kwa mwaka. Hivyo mwaka mmoja unaingiza milioni nne na laki nane unaingiza, unasubiri nini rafiki yangu ajira serikalini ni shida tutumie fursa tulizonazo wenyewe. . Kwa mawasiliano zaidi whatsapp 0625728742

4 comments

Jamani Mimi ninamayai nauza kwamaeneo ya dar.popote nakuletea

Wohoooo like it 🙏💖💖🙏🙏

Nipo Unguja Zanzibar yai moja tsh 450 ni la kuku wa kienyeji OG simu no. 0777345317

Nitafute kama unataka mayai , kutoka kijijini ya kienyeji
0654111149


EmoticonEmoticon