Friday, August 25, 2017

BOB JUNIOR AMLILIA DIAMOND PLATINUM

Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania na mmiliki wa Studio ya Sharobaro Records anayekwenda kwa jina la Bob Junior ambaye kwa wanaokumbuka vizuri sana huyu jamaa na Studio yake ndiye aliyemtoa Diamond na kumfanya kujulikana vizuri katika ulimwengu wa muziki. Na wote ni wajanja wa mitaa ya Tandale Dar es Salaam. Kamwambie Ulikuwa ndo wimbo wa Taifa kwa wakati ule na kwa sasa ungekuwa ndiyo jiwe la mwezi ndani ya Clouds radio, hakika ni wimbo ambao ulimtambulisha vizuri Diamond na hii ni kutokana na vinanda ambavyo vilipigwa vizuri ndani ya Sharobaro Record. Kama unavyojua tena barabara haikosi kona, kuna kipindi hawa jamaa waliwahi kupishana hali ambayo ilipelekea Diamond kutafuta Lebo nyingine ya kurekodi na kusimamia kazi zake, kumbuka akiwa Sharobaro hakuwahi toa hata senti mbovu kulipia muziki wake. Hivyo hali ya kutoelewana iliendelea mpaka walipokuja kukaa na kuondoa tofauti zao. Pamoja na kuondoa tofauti zao lakini hawakuwa karibu kama zamani na hii ni kutokana na Diamond kuwa bussy na harakati zake za kimuziki, hivi karibuni inasemekana Bob alimtafuta Plutnum ili amweleze tatizo lake na mtu pekee wa kumsaidia tatizo lake ni Diamond lakini hali imekuwa tofauti sana kwani wakipanga appointment lazima iyeyuke juu kwa juu, Bob anasema alipokuwa akitengeneza nyimbo za Diamond aliweza kupoteza uwezo kusikia vizuri kutokana tu na kumtafutia "blood" melody nzuri lakini Diamond huyo huyo kwa sasa hataki hata kuiona namba ya simu ya Bob Junior ikiita kwenye simu yake. Amesema haya alipokuwa akihojiwa na Kituo kimoja cha Luninga cha jijini Dar es Salaam.


EmoticonEmoticon