Friday, August 11, 2017

SIMBA SPORTS CLUB KUIKABILI MTIBWA SUGAR JUMAPILI

Tags

Timu ya soka S

imba itakuwa kibaruani tena siku ya jumapili ya tarehe 13-8-2017 kuikabili Mtibwa Sugar ya Tuliani Moro good. Mchezo huo utapigwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, utakuwa mchezo wa tatu toka walipotoka Afrika Kusini wa awali ukiwa dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ambao ulipigwa siku ya Simba day na Simba kuibuka na ushindi wa goli moja likifungwa na Mohammed Ibrahim na mchezo wa pili Ulikuwa dhidi ya Polisi Dar na matokeo yakiwa 2-1 Mavugo na Kazimoto wakiifungia Simba. Mchezo dhidi ya Mtibwa unakuja baada ya ule wa Singida United kuota mbawa. Mchezo huu utakuwa ni kipimo kwa timu zote mbili kujiandaa na ligi kuu msimu huu huku Simba ukiwa ni wa maandalizi kuelekea mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya timu ya Yanga ambao tayari wako visiwani Zanzibar. Baada ya mchezo huo dhidi ya Mtibwa utawapeleka nao Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kabla ya kuvaana na Watani wao wa jadi. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Manara.


EmoticonEmoticon