Sunday, August 27, 2017

IDRIS SULTAN KALETA KIATU KWA WATANZANIA

Mshindi wa Big Brother, Mtangazaji wa Choice Fm na Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idriss Sultan ameingia kwenye uzalishaji bidhaa ambazo ni muhimu kwa matumizi ya Watanzania hasa bidhaa za ambazo ni Viatu kwa vijana watanashati na wanaopenda kwenda na wakati. Hii inakuja baada ya msanii Diamond Platinum kuja na pafyumu ya CHIBU pamoja na KARANGA ambavyo vyote viko madukani kila Kona nchini Tanzania. Viatu hivi vyenye nembo ya Sultan vitakuwa sokoni muda si mrefu baada ya Uzinduzi wa bidhaa hii utakaofanyika tarehe 31-8-2017 jijini Dar es Salaam. Kitendo cha wasanii wa muziki na Filamu nchini kuingia kwenye ujasiriamali nje ya muziki ni darasa tosha kwa wasanii wengine kuiga hili na hata kwa watanzania wengine wasio wasanii kutafuta njia ya kuingiza kipato nje ya shughuli zao. Wasanii wengine walio katika biashara ni pamoja na WEUSI walio na bidhaa ya nguo, Ay aliye na bidhaa ya Kofia, ALI KIBA ambaye inasemekana muda si mrefu bidhaa yake ya nguo itakuwa sokoni. Wengine ni Dozen or B12 mtangazaji wa clouds redio ni miongoni mwa vijana wanaojishughulisha na utoaji wa bidhaa akiwa anauza nguo zenye nembo ya BORN TO SHINE. African boy "Jux" naye hayuko nyuma kutokana na uzalishaji na uuzaji wa nguo "t-shirt" zenye nembo ya AFRICAN BOY. Hivyo pongezi za pekee ziende kwao wote, Tumtakie maandalizi mema Idriss Sultan kuelekea uzinduzi wa brand yake mpya ya Viatu


EmoticonEmoticon