Baada ya kuhitimu Chuo niliamua kurejea kijijini ambako niliona ndiyo sehemu pekee ya kuutumia utaalamu wangu, kwa nilisomea masuala ya kilimo na mifugo katika ngazi ya diploma. Kama unavyojua ajira za siku hizi bila uzoefu kazini bado haujapata, hivyo sehemu pekee ya kunitoa hapa nilipo na kunipeleka ninapopataka niliona ni kijijini kwani sehemu pekee ambayo unaweza kulima na kufuga kwa gharama ndogo.
Nilifika kijijini ndani ya mkoa wa Njombe sehemu ambayo wazazi wangu walizaliwa na kukulia kabla ya kuhamia mjini. Wazazi wangu hawakuamini katika kilimo wao walijua ili ufanikiwe ni lazima uishi mjini hivyo walihamia mjini ambako walijishughulisha na biashara ndogo ndogo. Kwa kuwa habari ya kijijini hawakutaka kuisikia hata kidogo ilikuwa ngumu kwao hata kununua shamba. Nilifikia kwa mjomba wangu aliyekuwa akijishughulisha na kilimo cha nyanya pale kijijini, nashukuru alinipokea vizuri yeye na shangazi yangu. Niliwaeleza azma yangu pale kijijini baada ya kuhitimu kozi yangu ya kilimo na mifugo katika chuo cha kilimo maarufu nyanda za juu kusini kilicho katika mkoa wa Mbeya. Walionyesha kutokuwa na imani na mimi ukizingatia nimezaliwa mjini, nimekulia mjini, nimesoma mjini na maisha nikaanze kijijini lakini waliniahidi kunipa Sapoti kwa kadri watakavyo weza kwani mashamba wanayo mengi wakaniahidi kunipa kipande ndani ya mashamba yao. Nilifurahi sana na kuahidi kuwa sitowaangusha Kamwe na watafurahi uwepo wangu pale kijijini.
Siku moja asubuhi sana na mapema niliamka kufanya usafi wa uwanja, nikiwa nje nilisikia minong'ono ya mabishano baina ya mjomba na shangazi. Mabishano hayo yalinifanya nisogee dirishani kwao nisikie vizuri. Shangazi alikuwa akimwambia mjomba kuwa huyu binti yetu atatusaidia sana katika shughuli zetu pia lakini mjomba hakuonesha kuliafiki hilo zaidi akasema mikono yenyewe laini vile ataweza kazi kweli? Shangazi akajibu "mume wangu usimpime mtu kwa macho". Mjomba akakazia "labda si tupo tutaona". Nilitoka pale dirishani nikitafakari maneno yale ya wenyeji wangu, mjomba inaonesha hanikubali lakini shangazi ananikubali 'sasa nitawaonesha uwezo wangu' nilijisemea mwenyewe nikiendelea na kazi.
Maisha yaliendelea mbele nilianza kuzoea maisha ya kijijini. Siku moja tukiwa tunapata chakula cha jioni mjomba aliniambia kuwa kesho asubuhi tujihimu shamba ili nikaangalie eneo litakalonifaa kwa shughuli zangu za kilimo, kwa kweli nilifurahi sana usiku ule na kumuahidi mjomba wangu makubwa.
Tuliamka asubuhi na mapema kujiandaa kwa safari ya shamba tulifika mimi na mjomba hakika lilikuwa ni eneo zuri na lenye rutuba mpaka nikawafikiria wazazi wangu wanavyohangaika mjini ilhali kijijini kuna ardhi nzuri kabisa yenye rutuba ya kutosha. Tulizungukia maeneo yote ya shamba na mwisho tulifika eneo ambalo alinionyesha na kunikabidhi kuwa nitalima hilo na kwa kuwa Lina maji ya kutosha naweza pia fanya mradi wa samaki. Nilimshukuru sana mjomba na kumuahidi kutomuangusha.
Kwa kuwa tayari ilikuwa ni saa nane mchana, Mjomba aliniambia muda umeenda ngoja akakate ndizi za kurudi nazo anikute pale, nilimkubalia. Na kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana niliona nijipumzishe kidogo ninapomsubiri mjomba aje, nikiwa pale nimelala usingizi ulinipitia na kulala fofofo. Nilikuja pata fahamu usiku mnene baridi likiwa kali sana na nilipojikagua nikabaini nilikuwa uchi kama nilivyozaliwa huku mikono yangu ikiwa imefungwa kwenye mti na kadri muda unavyozidi ndivyo nilivyokuwa napata maumivu makali mwilini na ndipo nilipogundua kuwa nilifanyiwa mchezo Mchafu na mjomba baada ya kupata maumivu makali kutoka sehemu za siri na za haja kubwa kifupi aliniingilia mbele na nyuma. Nililia sana lakini sikupata msaada wowote za ya kuendelea kupata maumivu makali pamoja na baridi kali nilijuta kwa nini nilikuja kijijini kule. Kelele zangu za kilio zilimfikia mama mmoja ambaye alikuwa amewahi shambani alifika na kunifungua kamba mikononi na kunipa nguo zilizokuwa pembeni yangu zikiwa zimelowa damu na kunipa kitenge chake nijifunge wakati anafuata maji aje aninawishe ghafla alipiga kelele na kurudi nilipo kwa taabu nikamuuliza kulikoni, hakujibu zaidi ya kuonesha mkono alikotokea sikuelewa kitu.
Ndipo aliponifuata na kunieleza kuwa mjomba wako amekufa, sikumuelewa hadi aliponikongoja kunisogeza pale ilikuwa ni majonzi Nililia sana hadi fahamu kukata, nilipozinduka nilikuwa hospitalini nikiwa na dripu za maji pembeni akiwa amekaa mama yangu akiwa analia. Nilishangaa kumuona mama nikamuuliza nimefikaje pale akasema "uliletwa na wasamaria wema ukiwa hujitambui" nikamuuliza na mjomba yuko wapi mama akazidi kulia kwa kwikwi na kuniambia mjomba wako alijiua baada ya kukubaka na kukulawiti kuepuka aibu alijinyonga.... Mimi kusikia hivyo tena nilijikuta nguvu zikiniisha na taratibu nilipoteza fahamu.
Nilikuja zinduka baada ya siku tatu ambapo baada ya matibabu na taratibu zote kukamilika niliruhusiwa kurudi nyumbani, lakini mpaka muda huu siko vizuri kwani naongea kwa shida na ninatembea kwa taabu.
Ndoto zangu zimeyeyuka na nipo njia panda sijui maisha yangu yatakuwaje baada ya hapa na ninajiuliza kila siku kwa nini mjomba alinifanyia ukatili ule?
"MAISHA YANABADILIKA MUDA WOWOTE NA NDOTO ZINAWEZA FIKIWA AU ZISIFIKIWE. TUPAMBANE NA WAKATI TULIONAO" Mwisho
Saturday, August 12, 2017
STORI ITAKAYOKUTOA MACHOZI
Diterbitkan August 12, 2017
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon