Shirika la Wambea Duniani lenye Makazi yake jijini Dar es Salaam nchini Tanzania hivi karibuni wakiwa katika harakati za kutimiza Majukumu yao walikutwa na songombingo. Shirika hili ambalo kazi yake kubwa ni kutafuta habari za kweli lakini ambazo zimefichika kifupi ni zile za KIMBEA,viongozi wa kundi hili ni Soudy Brown na Qwisar. Hawa ni vijana ambao ni mahost wa kipindi hicho cha Shilawadu kupitia Clouds TV kinachorushwa siku ya Ijumaa.
Siku za hivi karibuni walipata taarifa kuwa Ali Kiba amerudi kutoka ziarani nje ya Tanzania, wakaona siyo kesi ngoja waende wakapate machache ni kwa nini ngoma mpya imechelewa kutoka na mashabiki wake wamechoka kusubiri. Mwaka umepita tangu alipotoa ngoma ya AJE. Hivyo katika kufuatilia issue hiyo walifika nyumbani kwa King Kiba lakini weeeeeee walichokutana nacho huko we acha tu, moja ni kususiwa nyumba na baadaye wakakamatishwa mbwa. Kumbe Soudy ana mbio? Ilibidi wasahau kilichowapeleka huko
Friday, August 18, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon