Tukiwa tunahesabu masaa kwa dirisha la usajili kufungwa, timu ya soka ya Singida United ya mkoani Singida iliyopanda daraja na kuingia ligi kuu msimu huu imenasa saini ya mshambuliaji hatari mwenye kucheka na nyavu MICHELLE KATSAVAIRO aliyekuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya KAIZER CHIEFS ya Afrika ya Kusini inayoshiriki ligi kuu ametua Singidani kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji baada ya kubaini haina makali ya kutosha ilipocheza na Yanga na kupoteza mchezo huo wa kirafiki kwa kupokea kichapo cha bao 3-2.
Baada ya usajili huu Singida United itakuwa ndo timu iliyofanya usajili mzuri wa kikosi chake kwa timu kutoka mikoani na kutumia kitita kikubwa cha fedha na hii ni kutokana na udhamini iliyo nao ambao ni zaidi ya wadhamini watano.
EmoticonEmoticon