Saturday, September 16, 2017

WATU WASIOJULIKANA WAVAMIA DUKA MJINI LUPA CHUNYA NA KUFANYA UHALIFU

Watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wamevamia duka la mfanyabiashara maarufu mjini Lupa Chunya ndani ya mkoa wa Mbeya  na kufanya uhalifu ikiwa ni pamoja na kufyatua risasi dukani hapo bado haijafahamika kama kuna mauaji yametokea, lakini Polisi wamefika eneo la tukio kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwatafuta Majambazi hao ambao inasemekana wametokomea kusiko julikana.Eneo hili la Lupa linapatikana katikati ya Makongolosi na Kambi katoto barabara iendayo Tabora na Singida.


EmoticonEmoticon