Saturday, September 2, 2017

VeeMoney na Jux kama zamani

Wasanii wawili wa Bongo fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee "VeeMoney" na African Boy "Jux" ambao kwa takribani miezi mitano hawako pamoja kimapenzi, kuna kila aina ya dalili wawili hawa wamerudiana japo bado hawajaweza kuweka wazi, hii inakuja kwa Jux ambaye amekuwa akitamani kuongea kitu lakini anashindwa na kuishia kusema hawawezi kurudiana ila atamlinda Vanessa. Tutarajie kitu kipya kutoka kwao baada ya Tour ya Tigo Fiesta 2017 inayoandaliwa na XXL ya Clouds fm radio kutoka Clouds Media Group. Hapa dalili za zilipendwa hakuna zaidi wamejaribu kuingiza kuachana wameshindwa sasa wanatafutia pa kuibukia... Na sisi tumeona hiyo na tunaifuatilia hii mpaka mwisho wake. Usisahau kuidownload application yetu ya SAYARINEWZ APPambayo inapatikana Google Playstore.


EmoticonEmoticon