Wednesday, September 13, 2017

MSONGAMANO WASABABISHA WAFANYAKAZI NA WANAFUNZI KUCHELEWA MBEYA

Tags

Jiji la Mbeya linakabiliwa na tatizo la msongama
no wa magari, adha hii imepelekea wafanyakazi na wanafunzi shule na vyuo kuchelewa kufika maeneo yao ya kazi na masomo. Hali hii inasababishwa na jiji la Mbeya kuwa na one way wakati jiji linaendelea kukua, hivyo halmashauri ya jiji inatakiwa kujipanga katika hili ili kuepusha msongamano kama ilivyo kwa majiji mengine kama Dar, Mwanza, Arusha na Tanga.
Kutokana na jiji la Mbeya kukua haraka barabara nyingi ndani ya jiji zinatakiwa na pia two way roads zinatakiwa ili kuendana na kasi. Barabara ya kuelekea Isanga kutoka Mwanjelwa inatakiwa kuwekwa lami. Hali kadharika barabara ya malori au magari ya mizigo inatakiwa ili kuyaondoa katikati ya jiji. 
Endelea kuwa karibu na blog yetu bila kusahau kupakua APP YETU YA "SAYARINEWZ" 


EmoticonEmoticon