Kinywaji cha Pepsi chaleta maswali na gumzo mtaani baada ya kutumika kusafishia betri za pikipiki, magari na solar. Kinachofanyika ni hiki,
Kwanza, kabisa mwaga maji yaliyokuwa yakitumika kwenye betri kisha liache juani likauke. Pili, chukua Chupa za Pepsi za kutosha weka kwenye kila tundu la betri Kinywaji hicho. Tatu, tikisa kwa nguvu betri hilo ili kuondoa uchafu na kuruhusu soda kupenya kwenye seli. Nne, mwaga uchafu huo chini na hakikisha betri inakuwa kavu kabisa. Tano, weka maji mapya kwenye betri hiyo kwa kiasi lengwa na kisha iweke juani ipate joto na chaji ya kuanzia. Sita, itoe iko tayari kwa matumizi. Ya gari ipeleke uchaji kwanza, ya sola kaiunge kwenye system ya solar tayari kwa matumizi.
Watu wanahoji ikiwa inafanya kazi ya kuamsha seli za betri vipi kuhusu afya ya mtumiaji? Haina madhara? Tafadhali tupe maoni yako ndugu msomaji katika hili.
EmoticonEmoticon